TASAF KUWANUSURU WAHADZABE

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) umeanza mkakati maalumu utakaowezesha jamii ya Wahadzabe walio katika mikoa ya Arusha,Manyara na Singida kuandikishwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na mfuko huo nchini kote.

Wakizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unavyotekelezwa katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha,viongozi wa TASAF walioambatana na wadau wa maendeleo walioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchi za Tanzania Bi. Bella Bird,na baadhi ya maafisa wa benki hiyo kutoka Marekani ,baadhi ya wahadzabe waliomba kuorodheshwa katika Mpango huo ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo kupitia utaratibu wa kuhawilisha fedha.

“ Baadhi ya wananchi wenzetu wameandikishwa kwenye mpango huku wengi wetu hatujapata fursa hiyo na tumeanza kuona namna wanavyonufaika na huduma za mpango huo’’ alisisitiza mmoja wa wahadzabe katika kijiji cha Endamaghan umbali wa kilometa 70 kutoka makao makuu ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Akizungumza baada ya kutembelea makazi ya wahadzabe Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- kwa kuweza kuwafikia wananchi ambao wanakabiliwa na umaskini nchini kote.

‘’Benki ya Dunia inatambua na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kukabili tatizo la umaskini miongoni mwa wananchi wake,umuhimu mkubwa pia unapaswa kuwekwa katika kunusuru jamii za watu walioko katika mazingira magumu wakiwemo wahadzabe” alisisitiza Bi. Bird.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-Bwana Ladsilaus Mwamanga alisema zoezi la kutambua na kuziandikisha kaya maskini katika jamii ya Wahadzabe lilifanyika. Hata hivyo alisema zoezi hilo liliathiriwa kwa kiwango kikubwa na mfumo wa maisha ya jamii hiyo wa kuhamahama kutafuta chakula kwa kuwinda wanyama na kuokota matunda na asali.

“Hatukuweza kuwaandikisha wote ingawa kimsingi wanastahili kuingizwa kwenye Mpango,hii ilitokana na kuhamahama kwa wananchi hao kujitafutia chakula hususani matunda, asali na mizizi” alisisitiza Bwana Mwamanga.

Hata Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameahidi kuwa kazi ya kuziandikisha kaya za walengwa katika jamii hiyo ya wahadzabe na nyingine zenye maisha ya kuhamahama itafanyika upya na kwa haraka ili waweze kuziingiza kwenye Mpango wa Kunusuru na Kaya Maskini unaotia mkazo katika kuboresha maisha ya walengwa hususani kupitia sekta za elimu, afya,lishe na kukuza kipato kwa kaya za walengwa.

Zifuatazo ni picha za ziara ya viongozi wa TASAF na Wadau wa Maendeleo katika maeneo ya wahadzabe,wilayani Karatu Mkoani Arusha.

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa Kaunda suti) akiwasikiliza baadhi  ya wananwake wa jamii ya Wahadzabe katika kijiji cha Endaghan wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo na TASAF kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .

pic2

Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi  Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird ( hayupo pichani) alipotembelea kijiji cha Endamaghan kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF.

pic3

Mmoja wa wananchi kutoka jamii ya Wahadzabe akieleza jambo kwa viongozi wa TASAF na Benki ya Dunia waliotembelea kijiji cha Endamaghan wilayani Karatu mkoani Arusha kukagua utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini. Wananchi hao wameomba kuingizwa kwenye Mpango huo ambao umeorodhesha baadhi yao kutokana na tabia yao ya kuhamahama na hivyo kuwa vigumu kuwapata

pic4

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird (watatu kushoto waliochuchumaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Endamaghan ambao ni wahadzabe ambao wameomba kuingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini fursa ambayo waliikosa kutokana na mfumo wao wa kuhamahama.

 pic5

Wananchi jamii ya Wahadzabe wakiwa mbele ya nyumba yao katika eneo la Endamaghan wilaya ya Karatu mkoani Arusha. TASAF inakusudia kuiorodhesha jamii hiyo katika mpango wa kunusuru kaya maskini.

pic6

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akiwahutubia wakazi wa Endamaghan katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha juu ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini (hawapo pichani) wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga.

 pic7

Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Endamaghan kutoka  jamii ya Wahadzabe  akipokea fedha za ruzuku kupitia mpango huo.

pic9

Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika kijiji cha Endamaghan wakiwemo jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (hayupo pichani) juu ya utekelezaji  wa  Mpango huo.

Opening event, Face-to-face Meeting of the Africa Community of Practice of Cash and Conditional Cash Transfers (CoP) Ngurdoto Mountain Lodge, Arusha, Tanzania

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

arusha1

The Vice President of the United Republic of Tanzania, Hon. Samia Suluhu Hassan delivering a speech during an opening of   Face-to-face Meeting of the Africa Community of Practice of Cash and Conditional Cash Transfers (CoP) at Ngurdoto Mountain Hotel in Arusha

aruha2Minister of state in the President's Office Public Service Management and Good Governance Hon.  Angella Kairuki addressing the CoP meeting at Ngurdoto in Arusha

arusha3

The Tanzania Social Action Fund-TASAF National Steering Committee Chairman Mr. Florens Turuka delivering a welcome remark to the CoP delegates.

arusha4The World Bank Country Director (Tanzania, Kenya Uganda and Burundi) Ms Bella Bird delivering remarks on CoP at Ngurdoto Hotel in Arusha

arusha5

The Executive Director of TASAF Mr. Ladislaus Mwamanga giving a vote of thanks after the Vise President Hon. Samia Suluhu Hassan opening speech during CoP meeting at Ngurdoto Hotel in Arusha

arusha6The UNICEF Deputy Representative in Tanzania Mr. Paul Edwards delivering a speech during CoP meeting at Ngurdoto Hotel in Arusha

arusha7

Part of delegates listening to the speech of The Vice President of the United Republic of Tanzania, Hon. Samia Suluhu Hassan at Ngurdoto Hotel in Arusha (not in the photo)

arusha9

Part of delegates listening to the speech of The Vice President of the United Republic of Tanzania, Hon. Samia Suluhu Hassan at Ngurdoto Hotel in Arusha (not in the photo)

arusha10Part of delegates listening to the speech of The Vice President of the United Republic of Tanzania, Hon. Samia Suluhu Hassan at Ngurdoto Hotel in Arusha (not in the photo)

arusha11

The Executive Director of TASAF Mr. Ladislaus Mwamanga speaking to media after an official opening of CoP meeting at Ngurdoto Hotel in Arusha

arusha12A group photo of CoP participants with Vice President Samia Suluhu Hassan (centre seated)