Installation Process

Download and install the Bundle file if Gantry is not installed, use the Standard Template file if Gantry is already present.

More Information

RocketLauncher - Demo Replica

Deploy a replica of this month's demo with ease, using the readily available RocketLauncher package.

More Information

Kundi la wadau wa Maendeleo Tanzania limevutiwa na mabadiliko chanya wanayoyapata walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya kukabiliana  na hali ya umaskini.

Hali hiyo ilijidhihirisha jana baada ya wadau hao wanaowakilisha mashirika, taasisi na mataifa mbalimbali yanayochangia maendeleo hapa nchini kutembelea katika vijiji vya Vikuge na Mwanabwito wilayani Kibaha na kuzungumza na walengwa, kushuhudia miradi waliyoianzisha na kupata shuhuda za hali halisi ya mabadiliko ya kimaendeleo kutoka kwa walengwa hao.

Wakiwa katika kijiji cha Vikuge, wadau wa maendeleo wanaojumuisha wakuu wa taasisi na mashirika kutoka Ubeligiji, Finland, Ujerumani, Ireland, Norway, USAID, AfBD, EU, UNRC, UNDP, UNWomen na Benki ya Dunia walipata nafasi ya kushuhudia bidhaa zinazotengenezwa kutokana na kazi za vikundi vya walengwa waliojiunga na kufanya shughuli za ujasiliamali kwa lengo la kujiongezea kipato.

Wadau hao pia walitembelea na kujionea utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Mwanabwito ambako walengwa wamepanda miti kuhifadhi chanzo cha maji katika bwawa wanalolitumia katika shughuli za uvuvi na kupata maji kwa matumizi ya nyumbani na kilimo.    

Zifuatazo ni picha zinazoonyesha matukio ya ziara hiyo:

 pic1

Sehemu ya viongozi wa kundi la Wadau wa Maendeleo Tanzania na uongozi wa TASAF ukiwasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya utambulisho

pic2

Sehemu ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Vikuge wakifuatilia taarifa mbali mbali zilizokuwa zikiwasilishwa mbele ya wageni (hawapo pichani)

pic3

Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa utambulisho wa wageni mbele ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Vikuge

pic4

Walengwa wa Mpango katika kijiji cha vikuge wakisoma shairi la ukaribisho wa wageni 

 pic5

Mlengwa katika kijiji cha Vikuge akitoa ushuhda wa namna alivyopata mabadiliko kutoka katika hali duni ya maisha na kufikia katika hali ya kumudu kugharamia maisha katika kaya yake

 pic6

Mmoja kati ya wadau wa maendeleo akizungumza na walengwa katika kijiji cha Vikuge

 pic7

Mkurugenzi wa Miradi ya jamii wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akifafanua suala kwa wageni

pic9

Ugeni ukiuliza maswali na kupata ufafanuzi toka kwa mlengwa waliyemtembelea kwenye Kaya yake kuona shughuli zake za ufugaji wa kuku na bata katika kijiji cha vikuge

pic11

Wadau wa Maendeleo wakitembelea shamba la miti iliyopandwa na walengwa katika kijiji cha Mwanabwito

 

 

 

 

 

 

Add comment


Security code
Refresh