User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze kutumia vyombo vya habari vilivyoko kwenye maeneo yao kutangaza habari za Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko huo

Akifungua mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa utaratibu wa Kikao Kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi ya kutokomeza umaskini nchini inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali vikiwemo  vyombo vya habari.

Bwana Mwamanga amesema tangu TASAF ianze kutekeleza Mpango wa kunususuru kaya masikini kumekuwa na mafanikio makubwa hususani katika maeneo ya walengwa ambao wameanza kuboresha maisha yao na katika baadhi ya maeneo walengwa wameanza kukuza shughuli za kiuchumi huku wengine wakiweza kuhudumia kaya zao  kinyume na hali ilivyokuwa huko nyuma.

Amewasihi waandishi wa habari kuwatembelea walengwa wa Mpango huo ili kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na Mpango huo wa uhawilishaji fedha na kisha kutangaza mafanikio yaliyokwishapatikana huku akisisitiza kuwa hata pale penye changamoto zionyeshwe ili maraekebisho yafanyike kwa manufaa ya walengwa .

Zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo kikuu Huria Mjini Mtwara

pic1

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Renatus Mongogwela (mwenye shati nyeupi)akizungumza na ujumbe wa TASAF ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Ladislaus Mwamanga wa kwanza kushoto kwa kaimu katibu tawala.

pic2

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga aliyesimama akifungua kikao kazi cha watendaji wa TASAF kutoka maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini na waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi (hawapo pichani)

pic3

Washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa TASAF na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)

pic4

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

pic5

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Add comment


Security code
Refresh